come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

YANGA YAIGOMEA SERIKALI

MABINGWA wa soka ligi kuu ya Tanzania bara ambao pia walikuwa mabingwa wa ukanda huu wa Arika mashariki na kati Yanga imesisitiza kuwa haitakwenda tena Sudan kufuatia kauli ya kwanza iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje Bernard Membe.


Akizungumza jana na mtandao huu, Baraka Kizuguto msemaji wa Yanga amedai tayari wameamua kuvnja kambi na kumruhusu kocha wake kurejea kwao Uholanzi, Huku ikiwaruhusu wachezaji wake wote na watarejea tena kambini mara baada ya kuanza tena ligi kuu ya bara.

Kitendo cha Membe kutoa tahadhali kuwa Sudan inakofanyika michuano ya kombe la Kagame si salama hivyo wamekubaliana na kauli ya mheshimikwa Membe, Suala la kuipeleka tena Sudan Yanga kwa sasa haipo alisisitiza Kizuguto.

Aidha Kizuguto ameshangaa kauli ya Naibu waziri wa michezo Amos Makalla kuziruhusu timu za Tanzania wakati muda wa maandalizi umekwisha na tayari walishatangaza kujitoa