Kwa mujibu wa baba yake Mangisemi Kileo alisema
mwili wa marehemu utaagwa kuanzia saa saba mchana nyumbani kwao
Mikocheni wakati mazishi yatafanyika saa 10 alasiri.
Kileo alisema mwanaye amefariki dunia kutokana na
kusumbuliwa na Malaria kali pamoja na uti wa mgongo, na kwamba juzi
alizidiwa ghafla wakamkimbiza katika Hospitali ya Kairuki, ambapo
walishauri apelekwe Muhimbili baada ya kugundulika na matatizo hayo.
“Tulilazimika kumkimbiza Muhimbili, ambako
alifikishwa katika chumba cha watu matuhuti (ICU), juzi ndiyo mauti
yamemkuta,” alisema.
Msanii huyo ambaye ni zao la Coca Cola Pop Stars
mwaka 2004, wakiunda Kundi la Wakilisha. Mbali ya Langa, wengine ni
Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwaijaga `Witness’.
Pia Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya (Tuma),
kimetoa pole kwa familia ya wasanii na kwamba tasnia ya
muziki nchini imepata pigo lingine tena kwani ni takribani muda wa wiki
mbili tangu msanii mwingine mahiri Albert Mangwea afariki Dunia.