.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema Tenga, ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ameitisha mkutano huo baada ya kupata maagizo kutoka Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA).
FIFA iliandika barua hiyo Aprili 29 mwaka huu iliyofuta kuvurugika
kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF na kuagiza kufanyika kwa
marekebisho ya katiba ya shirikisho hilo.
"Ajenda rasmi na taarifa nyingine zitatumwa kwa wajumbe siku 15
kabla ya Mkutano huo kwa mujibu wa Ibara ya 25(4) ya Katiba ya TFF.
Wanachama wa TFF ambao ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za
Ligi Kuu wanatakiwa kutuma majina ya wajumbe halali," alisema Wambura.
"TFF inapenda kuwakumbusha wanachama wake kutuma majina ya wajumbe
halali ili kufanikisha maandalizi ya Mkutano huo. Ni vizuri kuhakikisha
kuwa jina linalotumwa ni la mjumbe halali wa Mkutano Mkuu kwa mujibu wa
Katiba ya TFF."
FIFA ilifuta mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF na kuagiza kufanyika
kwa marekebisho ya katiba ya shirikisho hilo ili kuingiza kipengele cha
kuwapo kwa Kamati ya Maadili baada ya wagombe wawili,
Jamali Malinzi (nafasi ya urais) na Maichael Wambura (makamu wa
rais) kuliomba shirikisho hilo kuingilia mchakato wa uchaguzi huo kwa
madai kuwa kanuni zilikiukwa.