Akiwa kwenye kipindi ‘Keeping Up With The
Kardashians’ utafurahi, lazima utapata mambo mapya na pia utamaliza siku
yako kwa furaha. Hiyo ni kwa kuwa Kim anafahamu kutawala televisheni.
Licha ya televisheni, mwanamke huyo pia ni mkali
kwenye mambo ya mitindo. Mbali ya hayo, dada huyo pia hutenga muda wake
kwa ajili ya kucheza filamu ambazo zimekuwa zikimpatia tuzo, mara kadhaa
amekuwa akitajwa kwenye makundi ya watu wanaowania tuzo mbalimbali.
Aanza kutikisa
Awali Kim alikuwa akifahamika kiasi tu, lakini
umaarufu wake ulipanda ghafla mwaka 2007. Jina la Kim lilikua baada ya
video yake ya ngono kati yake na Ray J kuonekana. Kampuni ya Vivid
Entertainment ndio ilisambaza nakala za video hiyo. Kim aliingia kwenye
mzozo mkubwa baada ya kuishtaki kampuni hiyo. Baadaye Kim alilipwa Pauni
5 milioni. Tukio hilo lilimfanya mwanamke huyo afahamike sana.
Baada ya muda kidogo alitikisa kwenye kipindi cha
‘Keeping Up With The Kardashians’. Kipindi hicho kimemnyanyua dada huyo
kwa kiasi kikubwa na kumpa fedha nyingi na analipwa Dola 400,000 kila
sura yake inapotokeza kwenye kioo.
Licha ya shoo hiyo, Kim ana vipindi vya ‘Kourtney
And Khloe Take Miami’, ‘Kourtney And Kim Take New York’, ‘Dancing With
The Stars’ na ‘Khloe & Lamar’ ambapo analipwa si chini ya dola
100,000 kwa kila kipindi.
Dada huyo ameanzisha kampuni ya nguo ya D-A-S-H
kwa kushirikiana na ndugu zake Kourtney na Khloe. Shughuli zote hizo
ndio zinamfanya aingize Pauni 40,000 milioni kwa mwaka.
Licha ya mafanikio makubwa kwenye kazi zake, Kim
Kardashian amekuwa hana msimamo kwenye mapenzi na amewahi kuolewa mara
mbili kisha kuachika.
Alianza kufunga ndoa na Damon Thomas mwaka 2000 na
akaachika miaka miwili baadaye. Mwaka 2011 alifunga ndoa na Kris
Humphries ambaye ni mchezaji wa mpira wa kikapu, ndoa hiyo ikadumu kwa
siku 72 tu.
Vyombo vya habari vilisema Kim alifunga ndoa na
kaka huyo kisha akamuacha kwa sababu alitaka umaarufu. Sasa dada huyo
ameangukia kwenye mahaba na Kanye West ambaye ameamua kuzaa naye.