Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameweka wazi kuwa beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ atacheza badala ya Aggrey Morris wakati Mwinyi Kazimoto akiziba pengo la Mrisho Ngassa.
Morris atakosa mchezo wa kesho dhidi ya Ivory
Coast utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwania
mchujo wa Fainali za Kombe la Dunia Brazili 2014.
Beki huyo wa kati anayekipiga na klabu ya Azam FC
anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye pambano la marudiano
dhidi ya Morocco mjini Marrakesh. Stars ikilala mabao 2-1.
Kwa upande wa Ngassa anatumikia adhabu ya kadi
mbili za njano alizopewa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ivory Coast.
Stars ikilala mabao 2-0 na ya pili akilimwa pambano la Morocco. Stars
ikifungwa mabao 2-1.
Kim aliuambia mtandao huu jana jijini Dar es Salaam
kuwa nafasi ya Morris atacheza Cannavaro wakati akilazimika kumtumia
Kazimoto kucheza nyuma ya Thomas Ulimwengu, huku Amri Kiemba akicheza
winga ya kulia.
“Nafasi ya Morris atacheza Cannavaro. Pia,
nitambadilisha Kazimoto kucheza nyuma ya Ulimwengu wakati Kiemba
atacheza pembeni, winga ya kulia.” alisema Kim na kuongeza.
“Nafikiri kukosekana kwao hakuwezi kuathiri timu kufanya vizuri.” alisisitiza.