IKIWA mazoezi ya klabu ya Yanga yakizidi kupamba moto chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa, nyota wa kimataifa wa timu hiyo raia wa Uganda Hamisi Kiiza na Emmanuel Okwi wamewasili tayari kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika michuano ya kimataifa na ligi kuu bara.
Okwi na Kiiza walikuwa katika mapumziko ya Mwaka mpya nchini Uganda ambapo kuwasili kwao sasa kunaweza kuing'arisha Yanga inayoendelea kujifua katika uwanja wa Bora Kijitonyama, baadhi ya viongozi wa timu hiyo walikwenda kuwalaki wachezaji hao jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa JNIA.