KLABU ya Chelsea iko tayari kutoa ofa ya pili ya kumsajili Wayne Rooney (Pichani).
Kocha wa Stamford Bridge, Jose Mourinho
bado anakaza masuli kumpata mshambuliaji wa Manchester United na
ananiandaa kulipa Pauni 30 kukamilisha dili hilo.
Chelsea iliwasilisha ofa ya awali wiki iliyopita, lakini ikakataliwa na klabu ya Old Trafford.
United ilikataa pofa ya Pauni Milioni 23
taslimu jumlisha Milioni 2.5 malipo ya ziada ikisistiza Rooney, mwenye
umri wa miaka 27, hauzwi.
Chelsea inafurahi kumpa mshahara wa
Pauni 240,000 Rooney kwa wiki anazolipwa United na watampa Mkataba wa
miaka mitano kama atafanikiwa kulazimisha kuondoka kwa mabingwa hao wa
England.
Rooney ambaye mambo yake hayajaeleweka
anafanya mazoezi viwanja vya mazoezi vya United, Carrington baada ya
kurejea kutoka kwenye kambi ya klabu kujiandaa na msimu kwa sababu ya
kuumia nyama.
Matarajio: Jose Mourinho anataka kumsajili Wayne Rooney Chelsea
Kipindi kigumu: Mustakabali tata wa Rooney unampa wakati mgumu David Moyes katika siku zake za mwanzo kazini United
Kocha wa United, David Moyes ameendelea
kusistiza Rooney, ambaye amebakiza miaka miwili katika mkataba wake Old
Trafford, hauzwi.
Lakini anaweza kupambana sana kumbakiza mchezaji huyo, kwqa sababu Mourinho anamtaka kweli Rooney na anapambana kumpata.