come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

COUTINHO AMFUNIKA SUAREZ THAILAND

Phillipe Coutinho

Nyota wa Brazil Philippe Coutinho aling’ara kushinda straika anayetaka kuondoka Luis Suarez kwa mchezo stadi wakati wa ushindi wa Liverpool wa 3-0 dhidi ya Thailand Jumapili.

Kiungo huyo wa kati ambaye ni mshambuliaji alifungua ukurasa wa ufungaji wa mabao kipindi cha kwanza kwa bao la juhudi za kibinafsi na alimwandalia fowadi kutoka Uhispania Iago Aspas kufunga la pili la Liverpool muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza.
Nahodha Steven Gerrard alifunga la tatu na pia akagonga mlingoti huku timu hiyo ya Brendan Rodgers ikikamilisha ziara ya Asia kwa kutofungwa bao lolote mechi tatu.
Suarez, ambaye anatakiwa sana na Arsenal, alicheza nusu saa ya mwisho ya mchezo uwanja wa Rajamangala mjini Bangkok lakini hakufanikiwa kufunga licha ya kugonga mlingoti kwa mpira wa kichwa.
Both Coutinho, aliyejiunga na klabu hiyo kutoka Inter Milan Januari, na Aspas, aliyenunuliwa majuzi kutoka Celta Vigo, walifunga mabao yao ya pili ziara hiyo na kuongeza nguvu Rodgers kabla ya msimu.
"Ilikuwa mechi nzuri na kulikuwa na magoli matatu mazuri,” Rodgers alisema. “Kiwango chetu cha mchezo kilikuwa sawa. Nashukuru sana timu hiyo ya Thailand, walicheza vizuri sana.” Rodgers alisema Suarez bado “ana safari” katika kuhakikisha yuko sawa kucheza na kwamba atahitaji kuimarisha mazoezi yake msimu ukikaribia. "Suarez ni mchezaji wa Liverpool kabisa," akasema.
Liverpool walidhibiti awamu za kwanza za mchezo huku Fabio Borino akisaidia sana. Pasi safi kutoka kwa Glen Johnson ilimfikia mshambuliaji huyo wa Italia lakini kipa wa Thailand Sinthaweechai Hathairattanakool akaokoa.
Hata hivyo, Coutinho ndiye aliyetamba zaidi kwa pasi zake na kudhibiti mpira, na pamoja na Gerrard wawili hao walidhibiti safu ya kati.
Na kunako dakika ya 16, Coutinho alipata bao. Aliupata mpira, na kuwacheza madifenda wawili wa Thailand kabla ya kufunga, na kufurahisha sana mashabiki. Thailand waliachwa tu wakishambulia hapa na pale huku mshambuliaji wao nyota Teerasil Dangda akituma kombora nje karibu na mlingoti wa kulia.
Dakika chache baadaye, kombora la Sarawut Masook lilimlazimisha kipa mpya wa Liverpool kutoka Ubelgiji Simon Mignolet kufanya kazi ya ziada. Liverpool walianza kipindi cha pili vyema na baada ya dakika nne pekee, Coutinho alimpa mpira Aspas, ambaye alimaliza kazi na kufanya mambo 2-0.
Na dakika ya 59, Gerrard alisababisha shangwe kuu pale alipotoa kombora safi baada ya kupokea mpira safi kutoka kwa Aspas. Vigelegele vilimkaribisha Suarez alipoingia uwanjani kukiwa kumesalia nusu saa, sawa na alivyokaribishwa mapema wiki hiyo Melbourne.
Gerrard alifaa kufunga bao la pili baadaye, alipozuia mara ya kwanza na kipa lakini kombora lake la pili lilienda juu. Timu hiyo ya Thailand iliendelea kushambulia lakini haikupenya ukuta wa walinzi wa Liverpool ambao haujapenywa wakati wa ziara yao Asia, baada ya ushindi wa 2- Indonesia XI na Melbourne Victory.
Rodgers alisema Liverpool imepokea uungwaji mkono mkubwa wakati wa ziara hiyo kukiwa na zaidi ya mashabiki 95 000 waliojitokeza kuwatazama katika Uwanja wa Kriketi wa Melbourne na pia walifurika uwanjani Bangkok Jumapili.