come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NAPOLI YAMPA HIGUAIN MWANZO MPYA


Gonzalo Higuain

Kisa kingine cha kuhama kwa mchezaji kilifikia kikomo Jumamosi baada ya Gonzalo Higuain hatimaye kukamilisha shughuli yake ya kuhamia Napoli kutoka Real Madrid.

Mkataba huo, ambao thamani yake huenda ikapanda hadi Euro 40 milioni ($49.1 milioni, £31.9 milioni) kutegemea ufanisi atakaopata raia huyo wa Argentina akiwa Italia, unafaida sana kwa Madrid ambao walilipa tu Euro 12 milioni walipomnasa kiungo huyo akiwa hajapikwa 2006.
Higuain ameimarika na kuwa mmoja wa washambuliaji bora zaidi Ulaya akiwa amefunga mabao 121 akiwa Madrid.
Hata hivyo, kama ilivyo kawaida Real, mchezaji huyo wa umri wa miaka 25 hakupendwa sana Santiago Bernabeu, si na mashabiki wa klabu hiyo na pia si na rais wa klabu hiyo Florentino Perez.
Tatizo ambalo Higuain alimpa Perez lilikuwa kwamba hakuwa mmoja wa wachezaji 'Galactico' ambao alinunua akitumia mamia ya mamilioni ya Euro tangu kurejea na kuchukua hatamu katika klabu hiyo 2009.
Perez hata hivyo alipata saini ya mshindani mkuu wa Higuain katika mashambulizi, Karim Benzema, na kwa hivyo mara nyingi amekuwa akimtetea Mfaransa huyo badala ya Higuain licha yake kufunga mabao mengi ukilinganisha na mechi alizocheza tangu wawili hao wawe wachezaji wenza miaka minne iliyopita.
Sehemu moja ambayo kumekuwa na tofauti kubwa sana katika uchezaji wa Higuain na Benzema hata hivyo ni katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na ni ufanisi wake katika dimba hilo la Ulaya ambao ulimfanya asichukiwe kabisa na wapenzi wa Real.
Higuain amefunga mabao manane pekee katika mechi 48 za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya alizocheza, ukilinganisha na 19 ya Benzema kutoka kwa mechi 34 za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya alizochezea Real na 31 katika 54 kwa jumla katika mechi zote.
Raia huyo wa Argentina alilimbikiziwa lawama baada ya kukosa nafasi mbili za wazi mechi ambayo Real walibanduliwa michuano ya timu 16 bora mikononi mwa Lyon 2010 na aliangukiwa na hasira za mashabiki wa Bernabeu tena alipozomewa wakati wa mechi ya pili ya nusufainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund baada ya kushindwa kufunga alipopata nafasi mapema.
Kuzomewa huko na hali kwamba hulazimika kugawana nafasi za kucheza na Benzema kulimfanya aondoke jiji hilo kuu la Uhispania na alitangaza hadharani kwa vyombo vya habari kufuatia mechi ya mwisho ya Real msimu uliopita kwamba alikuwa akitafuta kwa kuhamia.
Hata hivyo, Higuan bado alihangaika msimu wa majira ya joto.
Kuhamia kwake Juventus na baadaye Arsenal kulionekana kuiva na kungemfaa zaidi kuliko Napoli, lakini mabingwa hao wa Italia na klabu hiyo ya Uingereza wote hawakufikisha bei ya mchezaji huyo wa Madrid.
Badala yake, ni Napoli ambao walikuwa tu wamepokea Euro 64 milioni kwa kuuza Edison Cavani Paris Saint-Germain, walioweza kutoa pesa zilizohitajika huku mapinduzi ya Rafael Benitez ya kutumiwa Wahispania kwenye klabu hiyo ya Italia yakiendelea baada tu ya kununua Raul Albiol na Jose Maria Callejon kutoka Real Madrid huku naye Pepe Reina akijiunga nao kwa mkopo kutoka kwa Liverpool mkataba ambao unatarajiwa kukamilishwa siku chache zijazo.
Huenda awe hakutaka kuhamia huko sana lakini ukiangalia kwa kina Higuain alipata alilotaka. Alipoongea na wanahabari mwishoni mwa msimu uliopita, alisema angeenda pahala ambapo “atapendwa.”
Kuwasili kwake wiki hii, mwanzo Roma na baadaye Naples, kumezua msisimko furaha kuu miongoni mwa mashabiki wa klabu hiyo.
Na uwanjani, Higuan ana alilotaka kwani baada ya kuondoka kwa Cavani ina maana kuwa bila shaka atakuwa fowadi wa kati wa kwanza wa Benitez.
Hili litampa muda mwingi wa kucheza na kuthibitisha ustadi wake na kuonyesha ni yeye na si Carlos Tevez, Sergio Aguero au Ezequiel Lavezzi wanashirikiana na Lionel Messi safu ya mashambulizi ya Argentina wakisaka Kombe la Dunia kwa mahasimu wao Brazil msimu ujao wa majira ya joto.