Uongozi wa klabu
ya Yanga leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu ya urushwaji wa
michezo yake ya Ligi Kuu katika kituo cha luninga cha Azam ambacho
kimeingia makubaliano na kamati ya Ligi Kuu kuonyeshwa michezo yote ya
ligi kwa kipindi cha miaka miatatu (3).
Akiongea
na waandishi wa habari mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji amesema
uamuzi wa kamati ya ligi kuingia mkataba na kituo cha Azam Tv bila ya
kuwashirikisha wahusika wenyewe ambao ni vilabu vishiriki haukuwa sawa.
Sisi
kama klabu ya Yanga tulikaa kikao cha kamati ya utendaji na kuona
taratibu za kupewa haki ya matangazo kwa kampuni ya Azam haikua sawa,
sisi viongozi wa kalbu ya Yanga hatukushirikishwa katika mchakato huo
hivyo tukaona ni vema tuje kwa vyombo vya habari tuulezee umma juu ya
maazimio ya kamati ya utendaji.
Ifuatayo ni taarifa kamili kwa vyombo vya habari:
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
Hivi
karibuni, Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier
League chini ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo
Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake
kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam
Television (ambayo ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football
Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam
Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika
misingi ifuatayo:
1. BODI YA TPL
1.1 Bodi iliyoko
sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi
iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe ……….. mwaka
huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia
kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA
2.1
Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa
kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa
michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani.
2.2
Mfumo (undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha
mkataba kwa YANGA iachie urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na
Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya
Tanzania.
2.3 Makubalianokati ya TPL na Azam Television kuhusu
utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu zingine
zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania watapata mgao sawa wa
mapato ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu
kama inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau)
kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya
mwisho wa ligi.
2.4 Kamati ya Utendaji ya YANGA siyo tu
haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu
ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu
wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:
2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi;
2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama;
2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.
3. MIGOGORO YA MASLAHI
3.1
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa
Makampuni ya Azam na kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL
na Azam ni ya kutiliwa mashaka.
3.2 Makampuni ya Azam yana
yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa
vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu
zaidi kuliko mprira wa miguu, kama vile Azam F.C. hawashiriki katika
Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam
Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu
inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.
3.3
Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA
alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya
Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama
Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.
4. KUTOKUWA NA UWAZI
4.1
Mkataba wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na
ambao badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo
vingi vya habari, na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka
havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao
ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania
Premier League).
4.2 Ukosefu wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa
MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya
mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo kwaTPL.
5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA
5.1
Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa
Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na
siyo FIFA. TPL inasingizia kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia
kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali
"lock, stock and barrel."
5.2 TPL inaelezea kimakosa
makubaliano ya leseni ya urushaji wa mchezo ya mpira inayotarajia
kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini"
(“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa
michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano
na hivyo
wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.
Kwa
mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio
ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa
michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA Dar
es Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila
mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za
YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni
8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya
TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma
kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau
wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji) walikuwa wanaafikiana
kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati ya
Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara
yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo
makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya
Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.
Msisitizo
wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA
linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu
vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam
Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo
wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
......................
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013