|
|
Kigogo wa Manchester United Bobby Charlton anatarajia
mshambuliaji Wayne Rooney asalie kwenye klabu hiyo na anatumaini kuwa
ataendelea na kuvunja rekodi yake ya ufungaji mabao.
Hatima ya Rooney Old Trafford imekuwa haijulikani tangu mwisho mwa msimu uliopita pale kocha ambaye sasa amestaafu Alex Ferguson aliposema kuwa fowadi huyo wa Uingereza alikuwa amewasilisha ombi la kutaka kuhama.
Rooney alikanusha madai hayo lakini anadaiwa kuwa “mwenye hasira na aliyekanganyikiwa” na amekuwa akihusishwa na ofay a pesa nyingi kutoka kwa Chelsea. United wanasema hawana nia ya kuuza mchezaji huyo wa umri wa miaka 27.
Charlton, ambaye sasa ni mkurugenzi United, aliambia Sky Sports mjini Hong Kong, ambako klabu hiyo imo ziarani: "Wayne Rooney ni mchezaji wa Manchester United na nafikiri ataendelea kuwa mchezaji wa Manchester United.
"Huwa sipendi sana kupoteza wachezaji wazuri sana nay eye ni mchezaji mzuri sana.
“Nilikuwa natumaini kuwa siku moja huenda akafunga mabao mengi sawa na niliyofunga na ingekuwa vyema sana ikiwa alikuwa kwenye klabu yetu – na bado nafikiri hivyo.
Jeraha lilimfanya Rooney kuachana na ziara ya United ya kabla ya msimu Asia na Australia, lakini mkufunzi wa United David Moyes alisema mnamo Jumapili kuwa fowadi huyo yumo mbioni kurejea uwanjani kwa mechi ya kirafiki Sweden Agosti 6.
Mabao aliyofunga Rooney ni 197 na amepungukiwa na 52 pekee kuvunja rekodi ya Charlton ya kufungia klabu hiyo mabao mengi.