come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MRISHO NGASSA ATISHA KWA REKODI BONGO

KIUNGO mshambuliaji mpya wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga Mrisho Ngassa (Pichani), ameandika rekodi nne muhimu na za kihistoria katika maisha yake ya soka hapa nchini.


Ngassa aliyesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam ambayo ilimpeleka kwa mkopo Simba, Ameweka rekodi hizo kutokana na kutokuwepo kwa mchezaji aliyefanya vitu kama hivyo.

Rekodi yake ya kwanza ni kitendo chake cha kuichezea timu ya taifa kuanzia mwaka 2006 hadi sasa (2013) bila ya kushuka kiwango ama kutemwa hata mara moja.

Rekodi hiyo haijawekwa na mchezaji yeyote yule aliyekatika timu ya taifa hadi sasa, Huenda Shaaban Nditi angeweza kuwa sambamba na Ngassa lakini mkongwe huyo wa Mtibwa Sugar hayupo kwenye kikosi cha sasa cha timu ya taifa kinachonolewa na Mdenishi Kim Poulsen.

Ngassa ameandika rekodi nyingine ya kucheza vilabu vyote vitatu hapa nchini ambavyo ndivyo vikubwa, Ngassa ameichezea Yanga kisha akajiunga na Azam na Simba.

Rekodi nyingine ya Ngassa kurejea tena katika klabu yake ya Yanga ambayo alianza nayo kabla hajenda Azam, Ngassa pia ni mchezaji pekee nchini kucheza mechi na kikosi cha Manchester United wakati alipokwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Marekani