KLABU ya Liverpool imeanza harakati za kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa (Pichani) mmoja kati ya wachezaji ghali katika historia yao.
Wamepeleka ofa ya Euro Milioni 25 (Pauni
Milioni 21.85) kumnasa Costa, wakilenga kumfanya mwanasoka huyo wa
kimataifa wa Brazil kuwa mchezaji babu kubwa zaidi waliyemsajili majira
haya ya joto. Atletico sasa wanatafakari ofa hiyo.
Liverpool imekataa kusema lolote kuhusu mpango wa kumsajili Costa, mshambuliaji wa nguvu mwenye urefu wa futi 6 na inchi 2.
Iwapo dili hilo litakamalika, mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 24 ataingia kwenye orodha ya wachezaji wa
ghali wa klabu hiyo, akina Andy Carroll aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni
35, Fernando Torres Pauni Milioni 26 na Luis Suarez Pauni Milioni 22.8.
Brendan Rodgers anafanya jitihada za
kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Liverpool– lakini si kwamba usajili
wa Costa utafungua milango ya Luis Suarez anayetakiwa na Arsenal
kuondoka.
Rodgers anataka ushindani pale mbele
mwanzoni mwa msimu na haswa ikizingatiwa Suarez atakuwa anatumikia
adhabu katika mechi sita za mwanzoni na Daniel Sturridge, ambaye
hajacheza mechi yoyote ya kirafiki ya Liverpool anaendelea kupata ahueni
maumivu ya kifundo cha mguu.
Anabaki? Liverpool imesistiza Luis Suarez haondoki