Mwanadada Rose Ndauka amewawakia baadhi ya waandishi
wanoandika habari zauongo kuhusu yeye kufuatia hivi karibuni kuripotiwa
kuwa amekutwa kaitika nyumba ya wageni akivunja amri ya sita na
mwanamziki mmoja wa muziki wa kizazi kipya.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii Rose aliandika
“Dah magazeti yanapenda chokochoko kweli haswa wakimuona
mtu katulia....kama hujui uliza sio tu unaongea au unaandika kitu
ambacho ukijui......mnaudhi sana”
Huku akionesha picha ya gazeti moja la udaku lilikouwa na habari hiyo.
Hapo awali iliripotiwa na baadhi ya mitandao ya habari na baadhi
ya magazeti kuwa mwanadada huyu alionekana akipapaswa ndani ya gari na
baadaye yeye na mwanamuziki huyo aliyotajwa kwa jina la dogo Nasry
kwenda kuvunja amri ya sita katika hoteli ya chumba hicho.