come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

LIVERPOOL WAWASILISHA OMBI LA KUMNUNUA COSTA WA BRAZIL

Diego Costa

Liverpool wamewasilisha ombi la £21.8milioni kutaka kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid Diego Costa, Liverpool Echo walidai Alhamisi.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 24 anayechezea timu ya taifa ya Brazil atakuwa mchezaji wa tatu ghali zaidi kuwahi kununuliwa na klabu hiyo baada ya Andy Carroll na Luis Suarez.
Costa huenda hata akajaza vyema pengo la Suarez ambaye msimu wote wa majira ya joto amehusishwa na mipango ya kuhama Anfield katika juhudi zake za kusaka soka ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Costa alifunga mabao 20 katika mechi 44 alizochezea Atletico mashindano yote msimu uliopita.