come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

REAL MADRID YAICHAKAZA GALAXY


Luka Modric 

Mshambuliaji Mfaransa Karim Benzema alifunga mabao mawili kipindi cha pili na kusaidia Real Madrid kufagia Los Angeles Galaxy 3-1 mnamo Alhamisi katika dimba la kirafiki la Kombe la Mabingwa wa Kimataifa.

Angel Di Maria pia alifungia Real, bao lake la dakika ya 15 likiweka miamba hao wa Uhispania kwenye njia ya kupata ushindi wa nne katika miaka minne dhidi ya mabingwa hao watetezi mara mbili wa Ligi Kuu ya Soka.
Kufuatia ushindi huo, Real walijikatia tiketi ya pambano dhidi ya klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Everton katika kundi la washindi kwenye dimba hilo mnamo Jumamosi katika uwanja wa Dodger Stadium mjini Los Angeles.
Upande wa walioshindwa, katika ngome hiyo ya klabu ya besiboli ya Dodgers, Galaxy – ambao walipata bao la kupenmdeza kutoka kwa Jose Villarreal – watakutana na Juventus ya Italia katika kundi la kufutia machozi.
Dimba hilo, ambalo pia linashirikisha Chelsea, Inter Milan, AC Milan na Valencia litalmalizikia Miami Agosti 7.
Real Madrid walidhibiti mchezo kuanzia mwanzo, na Galaxy hawakuwezana na kasi yao na ustadi.
Cristiano Ronaldo aligonga mlingoti wa juu kwa mpira wa kichwa dakika ya sita, na chini ya dakika mbili baadaye kombora la Denis Cheryshev likaokolewa na kipa wa Galaxy Brian Rowe.
Real Madrid walienda kifua mbele dakika ya 15 pale Francisco Alcaron alipotwanga mpira kutoka kwa nusu yake na ukampata Ronaldo, ambaye aliwakwepa madifenda watatu na kumsambazia mpira Di Maria aliyeutuma nyumbani.
Ingawa aliendelea kutatiza kipa wa Galaxy, Ronaldo hakufunga. Aliondoka mchezoni wakati wa msururu wa kubadilishwa kwa wachezaji muda wa mapumziko ambapo Benzema aliingia uwanjani, na akafunga dakika sita tu baada yake kuingia.
Los Angeles walikuwa bila Landon Donovan na Omar Gonzalez, waliocheza mechi ya Jumatano katika timu ya MLS All-Star dhidi ya Roma ya Italia, na pia hawakuwa na Robbie Keane anayeuguza jeraha.
Hata hivyo, walifanikiwa kufunga la kuwafutia machozi dakika ya 63 pale Villarreal alipopata mpira ulioondolewa kutoka eneo la hatari la Madrid, akajipinda na kutuma kombora la guu la kushoto ambalo liliingia karibu na mlingoti wa kulia.
Benzema alirejesha uongozi wa Real wa mabao mawili dakika ya 74 kwa kufunga kwa kichwa mpira alioandaliwa na Di Maria.