come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SPURS YAPATA SAINI YA SOLDADO



Tottenham Hotspur wameafikiana na Valencia kuhusu ununuzi wa mshambuliaji Roberto Soldado na watalipa ada ya kuondoka kwa mchezaji huyo ya euro 30 milioni ($39.84 milioni), klabu hiyo ya La Liga ilisema mnamo Alhamisi.

“Valencia wamefikia makubaliano na Tottenham Hotspur Football Club, kusubiri kufanywa kwa uchunguzi wa kimatibabu, ya kuhama kwa Roberto Soldado kwa kiasi ambacho ni sawa na ada yake ya kuondoka ilivyo kwenye mkataba,” klabu hiyo ilisema kwenye tovuti yake (www.valenciacf.com).
Msemaji wa Valencia aliambia Reuters kuwa ada yake ya kuondoka ni euro 30 milioni, na ununuzi huo utavunja rekodi ya klabu hiyo ya London kaskazini.
Spurs walitumia pauni 17 milioni ($25.94 million) kumnasa kiungo wa kati wa Brazil Paulinho kutoka Corinthians mwezi uliopita, kiwango cha rekodi sawa na walicholipa Blackburn Rovers kumpata winga David Bentley mwaka 2008.
Rais wa Valencia, Amadeo Salvo, alsiema mnamo Jumatano kwamba mkataba umeingiwa tayari lakini kuna mambo kadha ambayo hayajakamilishwa hadi tatizo ndogo na maajenti wa mechaji huyo litatuliwe.
"Klabu hii ingependa kumtakia Roberto kila la heri katika awamu hii yake mpya ya uchezaji na tungependa kutaja utaalamu wake wa uchezaji stadi wa mwanasoka huyo katika mechi ambazo amevalia jezi ya Valencia," klabu hiyo ya La Liga iliongeza.
Soldado ambaye ana umri wa miaka 28, alifunga mabao 30 katika mechi 46 alizochezea Valencia msimu uliopita, ni mmoja tu wa wachezaji wa kimataifa wa Uhispania wanaoondoka nchi yao ya kuzaliwa kwenda kucheza Ligi Kuu ya Uingereza.
Wachezaji wanane kutoka kwa kikosi cha Uhispania kilichoshiriki Kombe la Confederations watakuwa Uingereza msimu ujao, idadi ambayo imepanda sana miaka ilivyosonga.
Mchezaji mmoja ambaye huenda akaelekea upande kinyume ni fowadi wa Tottenham Gareth Bale, ambaye anahusishwa na klabu ya Real Madrid.
Ripoti katika vyombo vya habari zinasema miamba hao wa Uhispania wameahidi kulipa ada ya kihistoria duniani ya zaidi ya pauni 85 milioni kwa kiungo huyo wa kati wa Wales wa umri wa miaka 24.
Soldado alianza uchezaji wake katika timu B ya Real Madrid ambapo alifunga mabao 63 katika mechi 120 alizocheza ligini.