Mchezaji aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni
48.6 majira haya ya joto, Neymar alianzia benchi dhidi ya klabu yake
hiyo ya zamani, sambamba na nyota anayetakiwa na Manchester United, Cesc
Fabregas, ingawa kiungo huyo wa zamani wa Arsenal alifunga mabao mawili
alipoingia kipindi cha pili.
Alexis Sanchez, Pedro na Lionel Messi
kila mmoja alifunga bao moja kipindi cha kwanza, wakati bao la kujifunga
la Leo, na mabao ya Adriano na Jean Marie Dongou, na mawili ya Fabregas
yalihitimisha karamu hiyo ya mabao.
Mabao ya mwisho? Nyota anayetakiwa na
Manchester United, Cesc Fabregas alianzia benchi lakini akafunga mabao
mawili kipindi cha pili
Messi (kushoto), Pedro (katikati) na Sanchez (kulia) waling'ara
La kwanza kati ya mengi? Barca imetwaa taji la Joan Gampar
Kasheshe: Neymar akilindwa dhidi ya shabiki mwenye hasira wa Internacional mjini Barcelona
Kocha mpya, Tata Martino (kulia) akimpa maelekezo Neymar