come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SIMBA YAUMBUKA KWA OLOYA, ATUMA SALAMU, ADAI ANATAKA KUCHEZA YANGA ILI ACHEZE MICHUANO YA KIMATAIFA

KLABU ya Simba imeshindwa kujiakikishia kumpata mshambuliaji hatari wa Uganda, Moses Oloya (pichani) ambaye walitangaza kumsajili katika kikosi chao msimu huu, Hata hivyo Mganda huyo amethibitisha kuwahi kufanya mazungumzo na Yanga na kulipiwa tiketi ya ndege.


Mtandao huu unaamini kuwa Oloya atakuja nchini kujiunga na Yanga kwani tayari wameoinyesha nia ya kumhitaji na tiketi ya ndege wamemtumia, Viongozi wa Simba walianza kumsaka Oloya muda mrefu ahata dirisha la usajili halijafunguliwa lakini walishindwa kumpata kutokana na dau lao dogo.

Yanga imefika muafaka na mchezaji huyo ingawa mpaka sasa ajaweka wazi kutua kwake, Lakini taarifa tulizonazo kuwa Oloya anaisubiria makataba umalizike ili ajiunge na kikosi hicho cha Yanga ambao pia ni mabingwa wa soka nchini.

Oloya anafanana sana Luis Suarez ambaye anataka kuondoka Liverpool na kujiunga Arsenal ili aweze kucheza michuano ya kimataifa, Na Oloya iko hivyo hivyo anataka kuichezea Yanga ambayo inasifika kwa kulipa vizuri mishahara ya wachezaji wake na itashiriki michuano ya kimataifa mwakani