Rais mteule wa Iran Hassan
Rouhani anaapishwa katika sherehe mjini Tehran ambapo atapewa idhini ya
kiongozi wa kidini nchini humo, Ayatollah Ali Khamenei.
Wakati wa kampeni zake rais huyo mteule aliahidi kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi, na alisema ataimarisha uhusiano kati ya taifa hilo na jamii ya kimataifa ambao uliharibika zaidi wakati wa utawala wa Rais Mahmoud Ahmedinejad.