KLABU ya Chelsea inajiandaa kupeleka ofa
ya pili ya Pauni Milioni 40 kwa ajili ya mchezaji wa Manchester United,
Wayne Rooney — na mshambuliaji huyo wa England ataingia kwenye nafasi
ya kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza la Jose Mourinho Stamford Bridge.
United sasa tayari imekwishakataa ofa ya
Pauni Milioni 30, lakini Mourinho ameweka wazi mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 27, Rooney ni chaguo lake la kwanza katika usajili huu.
Rooney ataonekana hadharani kwa mara ya
kwanza akiichezea United tangu Mei 5 nchini Sweden Jumanne katika mchezo
wa kirafiki wa kujiandaa na msimu dhidi ya AIK Stockholm, na atarejea
Old Trafford katika mchezo wa kumuaga Rio Ferdinand dhidi ya Sevilla
Ijumaa.
Kocha mpya? Jose Mourinho yuko tayari kumfanya Rooney mpiganaji wake mkuu safu ya mbele ya Chelsea
Alicheza kwa dakika 45 dhidi ya Real
Betis jana mechi ambayo mashabiki hawakuruhusiwa kuingia Uwanja wa
mazoezi wa Carrington ikiwa ni mara ya kwanza kuitumikia timu hiyo tangu
aumie nyama za paka katika ziara ya Asia.
Lakini hadi sasa, Rooney hajatoa ombi
rasmi la kuondoka licha ya David Moyes, kocha mpya wa United kuweka wazi
Robin Van Persie ndiye mshambuliaji wake mkuu.
Rooney anataka kucheza mfululizo na
anapenda kucheza pia kama mshambuliaji mkuu na vyanzo vinasema Mourinho
anaweza kumpa uhakika huo.
Namba 1: Moyes ameweka wazi kwamba Robin van Persie ni chaguo la kwanza katika ushambuliaji United msimu ujao