Mkuu wa sera ya kigeni katika Muungano wa Ulaya, Catherine Ashton, amekutana na Rais aliyeng'olewa mamlakani Mohammed Morsi.
Msemaji wa Bi Catherene Ashton, alisema kuwa mkutano ulifanyika katika eneo lisilojulikana ambako Morsi anazuiliwa na kuwa ulidumu kwa masaa mawili.
Hakutoa maelezo kuhusu walichokijadili.
Bi Ashton aliyewasili mjini Cairo siku ya Jumapilia, anatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari baadaye leo.
Hata hivyo tayari ameshakutana na maafisa kadhaa wa serikali akiwemo rais wa muda Adly Mansour, mkuu wa majeshi, Generali Abdel-Fattah al-Sisi na makamu wa rais wa maswala ya kigeni,Mohamed ElBaradei. Alisema kuwa atatoa wito kwa pande zote mbili kuhusishwa kwa serikali.