come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SHILOLE AMVAA SINTA, ATANGAZA BIFU DHIDI YAKE

MWIGIZAJI wa filamu na mwanamuziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (Pichani) amemtangazia ‘bifu’ msanii mwenzake na mtangazaji wa runinga, Christina John ‘Sintah’ kuwa atakapomkuta lazima ampe kipigo.


Shilole, alifikia hatua hiyo kwa madai Sinta kamponda katika mitandao ya kijamii.

“Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez), kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya ‘shoo’ Marekeni?” alihoji Shilole akinukuliwa na mtandao mmoja na kuongeza kuwa sasa ninachomwambia, ninamtafuta, nikikutana naye nitampa kipigo cha mbwa mwizi.

Katika mtandao wake, Sintah aliandika kuwa; Shilole ni sawa na mtu anayeota ndoto za mchana na kuwa aendelee kuota, anaweza baadaye kurudi katika hali yake.

Maneno yaliyomkera Shilole ni haya: “Shilole bwana, hii week katujia na kali kuliko, eti ameongea na Benny Medina (JLo’s Manager), ili aweze kufanya collabo na my sister, heee yes inawezekana maana hakuna lisilowezekana chini ya jua, lakini swali ni wataimbaje? Yule dada yake na mie ni RnB na music wa Shilole bado sijaujua ni chakacha ama nini, sasa naomba msaada kwenye tuta wadau wa music, hili lina uwezekano?

“Chakacha na RnB? Kwa sababu Shilole nyimbo zake sawa na Snura wa Majanga, kidogo Linah angeniambia ana collabo na my sisy ningeelewa, sasa Shilole? Ndoto za mchana ila si vibaya kuota maana ukishtuka unarudi katika reality.”

Shilole alisema hajawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama Sintah, anajifanya anambabaikia J-Lo wakati hata hajulikani, ameshangaa watu wa Bongo kuwa na tabia ya kudharau muziki wa nyumbani na kubabaikia muziki wa Marekani, wakati wenyewe hawana muda na muziki wa Bongo.

Aliongeza kuwa anamchukia Sintah kwa kuzungumza kitu asichokijua na kumponda yeye na Snura.

“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-Lo kuimba naye, lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu, alikubali kufanya kazi na mimi, ilitakiwa nionane naye Jumapili, lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?” alihoji Shilole.