Wabambe wa soka hapa nchini na mabingwa wa Ligi Kuu Kenya,
Tusker FC ndio wamiliki wapya wa Kombe la KPL Top 8 baada ya kunusurika
makali ya Thika United 5-3 kupitia mikwaju ya penalti katika fainali ya
kata na shoka ugani City Stadium, Jumatano.
Mechi hiyo ya kusisimua ilitamatika pande zote nguvu sawa 2-2 baada ya muda wa kawaida na ule wa ziada kabla ya hatima ya kikombe na kitita cha shilingi milioni moja kwa washindi kuamuliwa na karata ya penalti.
Kiungo Khalid Aucho alifanikiwa kuziba mkwaju wa tano na mwisho kuwapa Tusker ushindi baada ya Ezekiel Odera, aliyechapa wa pili kwa upande wa Thika kukosa pale juhudi yake hafifu ilipomezwa na kipa wa wanabia, Samuel Odhiambo.
Katika muda wa kawaida, mechi hiyo iliyoanza kwa kasi ilishuhudia bao la ufunguzi kutoka David Kingatua, aliyetia kimyani kwa njia ya ustadi wa kimataifa mnamo dakika ya 16 kufanya mambo 1-0 kwa faida ya Thika ambao hawajawahi twaa ubingwa wowote.
Tusker, ambao ni miamba wa kandanda nchini, walishinikizwa kujiinua na iliwachukua dakika nne pekee kusawazisha kupitia penalti pale Thika walipoadhibiwa kutokana na mpira wa mkono kwenye eneo lao la hatari.
Straika Ismail Dunga, alimlenga mlinda lando Lucas Indeche na kumwacha akitapatapa asijue mpira uko wapi.
Wafungaji hao, hasa Kingatua ndio walioibuka kama nyota wa fainali hiyo na katika dakika ya 23, mchezaji huyo wa Thika alimpata mwenzake na mshambuliaji wa timu ya taifa, Harambee Stars, Kepha Aswani lakini badala ya kupachika mpira wavuni, alipeperusha mkwaju wake nje na kupoteza nafasi murwa.
Katika kipindi cha pili, Kingatua aliachilia kombora lingine kali lililomlazimisha Odhiambo kulitema kwa taharuki ndani ya uwanja pindi majira yalipoginga saa tangu mechi kungoa nanga.
Asibaki kwenye giza, Dunga aliwatunuku Tusker uongozi wa 2-1 katika dakika ya 79 pale alipofikia pasi matata kutoka Aucho kabla ya Indeche kudaka mpira na kufedhehesha ngome ya Thika pale mpira ulipotiririka wavuni licha ya juhudi zao zote kuzuia bao.
Bila kukata tamaa, vijana hao walio onyesha mchezo wa kuvutia kwenye wingi, hasa ile ya kushoto, walijikakamua kwenye mashambulizi na wakafanikiwa kusawazisha dakika nne tu, kabla ya kipenga cha mwisho.
Kingatua aliweza kumuiga Dunga na kupata lake la pili alipofika kwenye eneo la hatari bila kupingwa na kusukuma mpira ndani ya neti kutokana na pasi nono kutoka kushoto.
Refa Moses Osano aliashiria muda wa ziada na dakika tatu baada ya mchezo kuanza tena, Dunga alikosa ulingo wa lango kwa hatua chache pale alipojipinda na kuchapa mpira huku ngome ya Thika ikisinzia.
Bila ya kusita, Kingatua naye alijibu hayo na kutuma mkwaju wa adhabu hatari kimo kiasi kutoka goli la Tusker.
Philip Opiyo alimfanyisha Indeche kazi ya ziada kabla ya kiungo wa Harambee Stars, Francis Kingatua kukamilisha nafasi za kufunga pale alipomsurutisha Odhiambo kuokoa mkwaju wake mzito.
Penalti zilipowadia, Dunga aliweza kumlemea Indeche kwa mara ya pili kufungua ukurasa kabla ya Vincent Omumbo kusawazisha. Kipa Odhiambo alimlagai mwenzake Indeche kuwapa Tusker uongozi wa 2-1 kabla ya kubadilika akawa shujaa kwa kumzuia Odera.
Ali Abondo, Collins Okoth na Aucho walikamilishia Tusker kibarua baada ya Sammy Meja na Simon Mbugua kupatia Thika matumaini.