KLABU ya Everton imekataa ofa ya Pauni
Milioni 28 kutoka Manchester United kwa ajili ya kuwanunua Leighton
Baines na Marouane Fellaini.
United imejaribu kumnunua kwa Pauni
Milioni 16 Fellaini - baada ya kukwama kuwanunua wachezaji wote kwa
Pauni Milioni 23.5 na kisha inajaribu pia kumnunua Baines kwa Pauni
Milioni 12, kwa mujibu wa gazeti la Liverpool, Echo.
Si ajabu, Everton imeipiga chini ofa
hiyo mara moja kutoka kwa kocha wao wa zamani, David Moyes, ambayo
ilipelekwa siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu England.
Wawili kwa mpigo: Kocha wa Manchester
United, David Moyes (chini) anajaribu kuwasajili wachezaji wa klabu yake
ya zamani, Everton, Marouane Fellaini (kushoto) na Leighton Baines
(kulia) wote kwa Pauni Milioni 28- lakini klabu ya Merseyside imepiga
chini ofa hiyo.
Ikiwa imekwama kuzinasa saini za Cesc
Fabregas, Thiago Alcantara na wachezaji wengine iliyowahitaji majira
haya ya joto, United sasa imeelekeza nguvu zake kwa wawili hao wa
Everton kuimarisha kikosi chake.
Lakini ofa kwa Fellaini na Baines
imeripotiwa kuwa chini ya thamani ya mchezaji huyo kwa kiasi cha Pauni
Milioni 10 ambayo Everton wanataka.
Sasa Moyes, aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson Juni, mwaka huu atatakiwa kujipanga upya.
Wamerudi kazini: Wote Baines (kushoto)
na Fellaini waliichezea Everton dhidi ya Norwich City katika sare ya 2-2
Uwanja wa Carrow Road Jumamosi