|
|
Chipukizi nyota wa Brazil, Neymar, alifunga bao lake la
kwanza la mabingwa wa Uhispania, Barcelona, pale walipowazaba Thailand
7-1 Jumatano.
Kiungo wa Taifa wa Uhispania, Pedro, alipata yake matatu huku nyota mkuu wa Argentina, Lionel Messi, alifunga mawili, moja kupitia penalti, katika onyesho lake la kipindi cha kwanza ambalo lilizua shangwe na nderemo kutoka mashabiki 50,000 waliojaza uwanja wa Rajamangala, Bangkok hadi pomoni.
Alexis Sanchez aliongezea wageni lao la saba na mwisho alipojumuika na mechi katika kipindi cha pili huku kocha mkuu mpya, Gerardo Martino akitizama vijana wake maarufu wakijitunuku ushindi wa kawaida dhidi ya wapinzani wao waliokosa makali licha ya juhudi kabambe.
Mshambuliaji wa taifa wa Thailand, Teerasil Dangda, alipachika bao la kufutia machozi katika dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza pale alipo lambishwa nyasi na mlinda ngome wa kutoka Cameroon, Franck Bagnack katika eneo la hatari.
Macho yote yaliangazia Neymar, ambaye aliripotiwa kuugua ugonjwa wa kukosa damu mwanzoni wiki hii na ushirikiano wake na mchezaji bora duniani mara nne, Messi, katika ushambulizi wa Barca.
Martino alisema wawili hao watasisimuka pamoja huku Barca wakipania muundo mpya katika mashambulizi ili kuondoa fedheha ya kuraruriwa na Bayern Munich katika kombe la kilabu bingwa barani Uropa msimu jana.
“Wao (Messi na Neymar) ni wachezaji tofauto lakini walionesha kuelewana leo,” kocha huyo wa zamani Paraguay alieleza wanahabari. “Walipatana vyema kabisa.”
Kiungo matata wa kati, Cesc Fabregas, ambaye amelengwa sana na mabingwa wa Uingereza, Manchester United, aliibuka kama kigezo cha juhudi zote zilizovutia za kusaka bao kwa upande wa Barcelona na kocha wake alisisitiza haendi popote.
“Fabregas yuko hapa nasi, anabaki nasi sasa na atabaki hadi mwisho wa mwaka,” Martino aliongeza akipuuzilia tetesi za uhamisho wake.
Kipindi cha pili kilishuhudia wachezaji wa kikosi cha kwanza wa Barca, Xavi, Andres Iniesta na Sergio Busquets wakiletwa mchezoni mahala pake chipukizi Sergi Roberto na Alex Song.
Barca wanasafiri Kuala Lumpur Alhamisi kucheza dhidi ya kikosi teule cha Malaysia Jumamosi.