come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TAARABT ATUA FULHAM KWA MKOPO

Adel Taarabt

Mchezaji wa timu ya taifa ya Morocco, Adel Taarabt atajiunga na klabu la Ligi Kuu Uingereza, Fulham kwa mkopo wa msimu mmoja kutoka Queens Park Rangers (QPR) ambao walishuka ngazi kutoka shindano hilo, waajili wake wapya walitangaza Jumatano.

Awali, kiungo huyo wa kati mshambuliaji alikopeshwa QPR na Tottenham Hotspur ambapo alicheza chini ya mwalimu wa sasa wa Fulham, Martin Jol, mwaka wa 2009 kabla ya kutia sahihi mkataba wa kudumu mwaka mmoja baadaye.
Taarabt ambaye alijiunga na safu za kulipwa na RC Lens mwaka wa 2006, alichezea Ufaransa kama chipukizi kabla ya kuamua kuwakilisha Morocco pale alipokomaa.
Fulham watafungua ligi ugenini Sunderland Agosti 17.