Gunners, waliofika fainali 2006 ambapo walishindwa na Barcelona 2-1, watasafiri Istanbul kwa mechi ya mkumbo wa kwanza ambayo itachezwa Agosti 20-21 kabla ya kurejea London kwa ya pili, iliyoratibiwa Agosti 27-28.
Kushiriki kwa Fenerbahce katika ngazi ya makundi hata hivyo kutategemea uamuzi wa Mahakama ya Uamuzi kuhusu Michezo, ambao unatarajiwa mwishoni mwa mwezi, baada ya timu hivyo kupigwa marufuku kutoka kwa dimba hilo la Ulaya na Uefa kwa kupanga mechi.
Hayo yajikiri, mabingwa mara saba AC Milan watakutana na timu iliyomaliza ya pili Uholanzi PSV Eindhoven – ambayo itakuwa marudio ya nusufainali ya 2004-05 ambayo Wataliano hao walishinda kwa mabao ya ugenini – nayo Lyon ya Ufaransa icheze dhidi ya Real Sociedad ya Uhispania.
Timu ya Ujerumani Schalke iliwekwa na Metalist Kharkiv ya Ukraine, ambayo inasubiri kusikiwa kwa madai ya kupanga mechi mbele ya Uefa Jumanne ijayo ambayo huenda hakaamua ikiwa itashiriki dimba hilo.
Upande wa mabingwa, mabingwa wa ligi Scotland Celtic walikabidhiwa Shakhter Karagandy, mechi ambayo itapelekea vijana hao wa Neil Lennon kusafiri kilomita 6 400 hadi Kazakhstan.
Droo:
Olympique Lyonnais v Real Sociedad
Schalke 04 v Metalist Kharkiv
Pacos de Ferreira v Zenit St Petersburg
PSV Eindhoven v AC Milan
Fenerbahce v Arsenal
Steaua Bucharest v Legia Warsaw
Dinamo Zagreb v Austria Vienna
Viktoria Plzen v Maribor
Ludogorets Razgrad v FC Basle Shakhter Karangandy v Celtic
Timu zilizotajwa kwanza zitacheza mechi ya mkumbo wa kwanza nyumbani. Mechi hizo za kwanza zitachezwa Agosti 20 au 21, nazo za mkumbo wa pili Agosti 27 au 28.