come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

PEP GUARDIOLA KUFANYIA MABADILIKO MAKUBWA BUYERN

Pep Guardiola
Guardiola aliongoza mechi yake ya kwanza kama mwalimu wa Bayern Ijumaa katika uga wa Allianz Arena, jijini Munich na alitumia dakika 71 akifoka maagizo kutoka eneo lake la kiufundi kati ya 90 za kivumbi hicho.


Mabao kutoka nyota wa Uholanzi, Arjen Robben, Mario Mandzukic wa Croatia na David Alaba wa Austria yaliwapa mabingwa hao watetezi alama tatu nyumbani.

Licha ya hayo, Guardiola alidhihirisha orodha kubwa ya maeneo Bayern wanatakiwa kuimarisha, jambo ambalo litawatia wasimamizi wa timu hiyo tumbo joto.

“Hatukuwa na msukumo tosha wakati mwingine, tuliwapa Gladbach muda mwingi na mashambulizi yetu ya mshtuko hayakwenda ilivyotakiwa wakati mwingine na tulipopoteza mpira, hatukurejelea nafasi zetu kwa haraka,” Guardiola alisema.

Bayern walifungwa mabao 18 pekee msimu jana- rekodi ya Bundesliga- lakini goli kipa Manuel Neuer alikuwa na kibarua cha ziada dhidi ya Gladbach.

“Nilikuwa na mengi ya kufanya,” kipa huyo wa Ujerumani aliye na uzoefu wa kutoshiriki pakubwa katika mechi wakati Bayern walitamba kwa kishindo msimu jana alikiri.

Guardiola ametupilia mbali mfumo wa 4-2-3-1 ambayo uliwaletea vikombe vya Ligi Kuu Bara Uropa, Bundesliga na Kombe la Ujerumani katika moja ya sababu inayoletea Bayern matata.

Badalake, kiungo wa Ujerumani, Bastian Schweinsteiger anatumiwa kama nanga ya eneo la kati mbele ya walinda ngome wane lakini kama Ijumaa ilivyodhihirisha, muundo huo unaacha nafasi kubwa.

“Pep si mwanamiujiza,” mkurugenzi wa michezo katika Bayern, Matthias Sammer, alisema lakini kikosi cha kocha huyo hakijarithika na mfumo wake mpya.

Guardiola mwenyewe alikiri ugumu wa kujieleza ipasavyo kwa wachezaji wake huku akiashiria anaweza kuondoa muundo wa 4-1-4-1.

“Wakati mwingine, ni vigumu kueleza wachezaji ninalolitaka kwa Kijerumani,” alisema. “Napenda mfumo huu lakini ni muhimu niwazoee wachezaji wangu na ninaweza kuubadilisha.”