|
Rooney ameripotiwa kusumbuka na hatima yake United na amekuwa chanzo cha maombi mawili ya kuhamia Chelsea yaliyokataliwa na klabu chake hivi majuzi.
Nyota huyo wa miaka 27 hajachezea timu yake hata dakika mojakatika harakati zao za kukaribisha msimu ujao lakini amesomwa katika kikosi cha Hodgson kitakacho menyana na majirani Scotland katika uwanja wa Wembley.
Mshambuliaji huyo wa zamani Everton alitumia ukurasa wake katika mtandao wa Facebook kumshukuru Hodgson akisema “Siwezi ngoja kuungana na kikosi cha Uingereza nikiwa na matumaini ya kucheza katika mechi shindani kama ilivyo kawaida dhidi ya Scotland.”
“Asante kwa Hodgson kwa kunichagua na kuonyesha imani na kuunga mkono kwake na ninashukuru.”
Magazeti ya Uingereza yalizua tetesi kwamba maoni hayo yanaweza chukuliwa kama kubeza Moyes lakini Hodgson alisema kuwa meneja huyo mpya wa United amerodhika na kuchaguliwa kwa Rooney.
“Shida iliyo hapa ni kuchagua Rooney kunaweza kutumiwa kama zozo kati yangu na Moyes,” Hodgson alieleza taarifa ya SkySports.
“Hakutakua na mtafaruku wowote kati yetu. Tumekua marafiki kwa muda mrefu na David anaelewa hali ya mambo.”
“David anafahamu yale tunayo kusudia lakini ni la kusikitisha na hatuna budi kukubali kwamba kutakua na maoni kadhaa kuhusu haya na wengine watajaribu kuzoa zogo lakini ni makosa kufanya hivyo.”
Gary Neville, nahodha wa zamani wa Rooney katika United na mshiriki wa kitengo cha ufundi cha Uingereza haamini kwamba tetesi kuhusiana na nyota huyo kutakua kutaathiri pakubwa kambi ya kikosi cha Uingereza.
“Hakutaathiri timu ya Uingereza. Nimecheza na Rooney kwa miaka mingi na nimekuwa kocha na Uingereza kwa mwaka mmoja na nusu uliopita,” aliongeza.
“Sijawahi kushudia akipatiana lolote ila asilimia 100 katika mazoezi na ni matusi kudhania atakua na athari zozote mbaya kwa kikosi cha Uigereza.”