Rais Obama amesema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili hauwezi kuendelea wakati raia wanauwawa.
Licha ya mauaji hayo na umwakikaji mkubwa wa
damu ,lakini kikao hicho cha dharura cha umoja wa mataifa
kilichoandaliwa mahusus kujadili swala la Misri kilikumbwa na mgawanyiko
mkubwa baina ya wanachama 15 wa baraza hilo la Usalama.
Kwa kawaida Urusi na China huwa zinapinga hatua yeyote ya baraza la usalama kuingilia maswala ya ndani ya nchi yeyote ile. Hivyo katika kikao hicho cha dharura , Urusi na China hazikibadili msimamo wao wa jadi , bado walipinga kuwa Misri na jeshi lisiingiliwe bali njia ya maridhiano itafutwe.
Pengine hii ni kutokana na swala la Chechnya ambalo bado linaisumbua Urusi huko China ikihangaishwa na tatizo la Tibet.
Taarifa zinasema China ilikataa katakata kutia saini taarifa rasmi ya baraza la usalama la kulishutumu jeshi la Misri kwa kusababisha umwagikaji wa damu na mauaji.