NAWEZA kusema Mrisho Ngassa ameonewa katima maamuzi yaliyotolewa dhidi yake yakimtaka ailipe klabu ya Simba shilingi milioni 45 kwa kutenda kosa la kusajili mkataba mpya na Simba akiwa kwa mkopo.
Turejee kwenye maamuzi ya kisheria hasa kwa watu wenye makosa ya ubakaji, Jamhuri ya muungano ilifanya marekebisho ya sheria ya ubakaji.
Zamani wenye makosa ya ubakaji waligundulika kimakosa ambapo utakuta mtu tu anapeleka mashitaka polisi kuwa amebakwa.
Na polisi kwa kutofuata sheria wamekuwa wakichukua sheria mkononi bila ya kufanya utafiti, Hapo ndipo idadi ya wafungwa wa makosa ya ubakaji walipoongezeka.
Na wengine walishitaki kubakwa na hatua kuchukuliwa, Utakuta mtu aliyebakwa ana umri mkubwa kumbe walidhulumiana tu na kumsingizia mwenzie amembaka.
Lakini faida ya marekebisho ilizaa haki, Umri ukawekwa kwa makosa ya ubakaji kuanzia mtoto wa mwaka 1 hadi miaka 17.
Pia kumuingilia kimwili pasipo makubaliano yoyote kwa watu waliozidi umri huo, Na kosa hilo litathibitishwa na daktari.
Adhabu yake ni kifungo cha maisha jela, Nani mbakaji, Mwanaume anatajwa kuwa ndiye mbakaji wa kwanza licha kwamba wapo wanawake wanaowabaka wanaume.
Wanaume ndio humtongoza mwanamke kwa kusudi la kufanya naye ngono, Hutumia kila namna kumshawishi ili mradi atimie kiu yake.
Na ikigundulika Anko Matua amefanya mapenzi na msichana mwenye umri wa kwenda shule basi anahisabika amebaka hata kama walikubaliana kwa hiari.
Hii inawazuia wanaume wenye tamaa ya ngono kutoshiriki mapenzi na wanafunzi, Sheria hii imekiukwa kwenye mchezo wa soka.
Simba imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja mchezaji aliye kwa mkopo, Simba ndio mwanaume ambaye ametumia mwanya huo kumtongoza mwanafunzi hata kama alimuonga fedha.
Sijawahi kusikia mahakamani hakimu akimuhukumu mtoto wa shule ambaye bado anaendelea na masomo kwa kufanya kosa la kushiriki mapenzi.
Kisheria yule mwenye uwezo wa kumrubuni mwanafunzi yule ndiye anahukumiwa kifungo, Ngassa ni sawa na mwanafunzi wakati Simba ni sawa na mwanaume mkorofi.
Simba ndiyo ilipaswa kufungiwa kwa muda wa miaka miwili na isijihusishe na usajili wowote wa wachezaji, Ngassa ana kosa lolote na alipaswa aendelee na hamsini zake.
Najua alirubuniwa na hongo, Isitoshe kumsainisha mchezaji aliye kwa mkopo ni kosa kisheria na mwenye makosa ni Simba.
Kupitia gazeti moja la michezo linalotoka kila siku ya Jumanne na Jumamosi lilionyesha mkataba wa Ngassa na Simba kuwa ulisainiwa mwezi Desemba mwaka jana kitu ambacho ni dhahili kosa la kisheria.
Ina maana Simba iliingia mkataba na Ngassa akiwa ndani ya mkataba wa mkopo, Adhabu gani ilistahili Simba kama si kufungiwa.
Umefika wakati sasa wanasheria wetu wanaoziongoza kamati mbalimbali za TFF kupitia vema vifungu vilivyomo ndani ya makaratasi yenu.
Kutumia ushabiki au kufunika kombe mwanaharamu apite mtindo huu umepitwa na wakati katika dunia hii iliyoendelea ya 'Kidijitali'.
Yanga haikufanya makosa kumsainisha Ngassa ambaye alikuwa mchezaji huru, Mkataba wa Ngassa na Azam ulimalizika mwezi Mei mwaka huu na Yanga ikaingia naye mkataba uliotambulika kisheria na TFF.
Kosa linakuja pale anapopewa adhabu ya kukaa nje kutoitumikia timu yake kisheria kwa mechi sita, Unajua Yanga imepata fedhea juu ya kutomtumia mchezaji wake!
Wanayanga sasa huu si wakati wa kulala ni wasaa wa kulilia haki yenu, Ikiwezekana kuishitaki kamati ya Mgongolwa kwa kosa la kuinyima haki Yanga kutomtumia mchezaji wake kisheria.
Simba imepewa kiburi na TFF na itaendelea na tabia ya kuwalaghai wachezaji kwa kigezo watakutwa na adhabu ya kufungiwa mechi sita huku wakifaidika na pesa ya dhambi ya fidia.
Simba inasema ilimlipa Ngassa milioni 30 ikiwa na kosa kufanya hivyo lakini inajikuta inapata milioni 15 za bure ikiwa yenyewe imefanya kosa tena kubwa, Itaendelea wiki ijayo