come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

WANACHAMA YANGA WAISHIO MBEYA LAWAMANI

Inasemekana kushindwa kupata ushindi katika mechi zake mbili zilizochezwa jijini Mbeya, kundi la wanachama wa Yanga wasihio jijini Dar es Salaam wam,ewalaumu wenzao wa Mbeya kwa kushindwa kutengeneza mazingira ya ushindi wakati timu hiyo ilipokuwa huko.


Kauli imetolewa na baadhi ya wanachama wa timu hiyo waishio jijini Dar es Salaam ambapo wamedai lawama zote wanazipeleka kwa wenzao wa Mbeya kwani wameshindwa kutengeneza mikakati ya ushindi, wanachama hao wameuambia mtandao huu kuwa watani zao Simba wapo makini na timu yao kuliko Yanga.

Simba ikienda mikoani hakuna hata shabiki anayeisaliti kuishangilia timu mwenyeji wote huwa kitu kimoja lakini anashangaa Wanayanga mkoani Mbeya wamejifanya Mbeya City au Prisons na kupelekea timu yao kuambulia pointi mbili badala ya sita.

Aidha wanachama hao wamejipanga kuipa nguvu Mbeya City katika mchezo wao wa leo na kudai hakuna hujuma zozote za kuidhuru timu hiyo iliyowapiga mawe jijini Mbeya, mwanachama mmoja ambaye amekataa kutaja jina lake amedai Yanga siku zote huishabikia mpinzani wa Simba hivyo leo watakuwa kwa Mbeya City