Ripoti kutoka Nairobi, Kenya,
zinasema kwamba watu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi katika eneo la
biashara katikati ya mji mkuu huo.
Inaarifiwa kuwa polisi waliobeba silaha wako katika eneo hilo.
Shirika la habari la Reuters linaarifu kuwa mpiga picha mmoja aliona watu wamelala chini tuli, hawatikisiki.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kama kuna watu waliokufa.