KITENDO cha uongozi wa Yanga kufanya mabadiliko ya sekretarieti ya klabu kimezua tafrani kubwa- na pamoja na wanachama kupinga, lakini pia kimeingilia mchezo wa kirafiki uliokuwa ufanyike Jumamosi kati ya klabu hiyo na Tusker ya Kenya.
Yanga imemuengua Katibu Lawrence Mwalusako na kuajiri Mtendaji Mkenya, Patrick Naggi na wanachama wa klabu hiyo wamepinga vikali hatua hiyo na kesho wamepanga kukutana na Waandishi wa Habari kuelezea msimamo wao.
Lakini pia, mchezo wa kirafiki baina ya timu hiyo na Tusker ya Kenya ulioandaliwa na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) hautakuwepo tena kwa sababu haijulikani nani ataidhinisha mechi hiyo baada ya mabadiliko haya na vurugu zinazoendelea.
Bosi mpya; Naggi ana uzoefu wa kuongoza soka Kenya, akiwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ligi Kuu Kenya, FKL.
Sasa DRFA imeamua kufuta kabisa ziara ya Tusker nchini ambayo ilikuwa pia icheze na Simba SC jumapili.