come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MIUJIZA: MZIMU WAMTOKEA BIBI ALIYEPOTEZANA NA NDUGUZE, SOMA MKASA KAMILI

Unaweza kudhania uongo kuhusu mkasa huu, lakini ndivyo ilivyo kwa bibi mmoja anayefahamika kwa jina la Bi Getrude Maranda (Pichani) mwenyeji wa Ifakara mkoani Morogoro ambaye ametokewa na mzimu wa marehemu babu yake usiku wa manane na kumtaka awatafute ndugu zake ambao hawafahamiani.


Akizungumza na Mambo Uwanjani kutoka Morogoro Bi Getrude Maranda amesema kuwa alitokewa na mzimu wa marehemu babu yake hivi karibuni akiwa amelala usingizini na kumtaka awatafute ndugu zake aliozaliwa nao ambao hawajui.

'Mzimu umenitaka niwatafute ndugu zangu ambao siwajui, aliniambia kuwa nilizaliwa na wenzangu wanne lakini hadi sasa niko peke yangu na wala sijawahi kuwaona, mzimu ukaniambia ndugu zangu wako Dar es Salaam na wanaishi Msasani na Kurasini', alisema na kuongeza.

'Hivyo nimeanza kutoa matangazo kupitia magazeti ili kuwapata ndugu zangu, ameniambia lazima niwapate na nikishindwa basi utakuwa mwisho wa maisha yangu, tena amesema ndugu zangu ni wa ukoo wa Maranda ambapo yule Askofu Marandu (Marehemu) pia ni ndugu yetu', aliendelea.

'Basi tangia hunitokee huo mzimu wa babu yangu nimeanza kuumwa tumbo, kichwa huku ukiendelea kunijia usiku, tena amenitajia na jina la ndugu zangu ila nimemkumbuka mmoja anaitwa Herman Maranda, popote anaposikia jina hili anitafute jamani nateseka', alisisitiza Bi Maranda.

Bi Maranda alitaja namba yake ya simu kuwa ni 0758 965976 au 0783 231441