come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TAMBWE ALIA UKATA LIGI DARAJA LA KWANZA

Kitwana Tambwe kipa wa JKT Kanembwa (Pichani) inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara amelia na ukata unaozidi kutishia maisha yake tangia alipojiunga na timu hiyo hivi karibuni.


Kipa huyo aliyewahi kuzitumikia Pan Afrika, Polisi Dodoma na Villa Squad ameelezea masikitiko yake kuwa tangia alipojiunga na timu hiyo inayotokea mkoani Kigoma ajalipwa pesa zake za usajili na kila anapoulizia napigwa kalenda.

Tambwe amesema kwamba yeye ana familia hivyo anashindwa kuisaidia kutokana na kuishiwa pesa za matumizi huku timu yake ikidai haina pesa kwa sasa na wachezaji waishi kwa uvumilivu, pia analia na kocha wa timu hiyo kwa kitendo chake cha kumweka benchi mara kwa mara.

Tambwe ni mmoja kati ya makipa waliojaaliwa miili ya kiuanamichezo na kupigiwa hesabu za kuwa tegemeo siku za usoni kwenye timu ya taifa, Taifa Stars, hadi sasa timu yake ya JKT Kanembwa imeonyesha dhamila yake ya kupanda ligi kuu mwakani