come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

OKWI AMPONZA MALINZI TFF, MASHABIKI YANGA KUANDAMANA.

Mashabiki  wa Yanga wameanza kulisakama na kulishinikiza Shirikisho la Soka (TFF) kuidhinisha usajili wa mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi katika klabu yao.

Januari 22 mwaka huu Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilitoa uamuzi wa kumzuia ilisimamisha usajili wa nyota huyo baada ya kubaini aliruhusiwa kuichezea SC Villa ya Uganda kwa kibali maalumu kutoka Shirikisho la Soka la Kimatiafa (Fifa).

Kamera za waandishi ziliwanasa baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi kushuhudia mechi yao ya raundi ya 16 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, wakibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali.


Mbali ya kubeba mabango hayo yaliyokuwa yamejikita katika kuishutumu Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF na baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu kisoka nchini, mashabiki hao pia walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali zilizolitaja jina Okwi na uongozi wa TFF.

Baadhi ya mabango yaliyokuwa yameandikwa kwa wino mweusi yalisomeka: "TFF tumechoka na fitina dhidi ya Yanga" na "Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji hatuna imani nayo".

Lakini, TFF kupitia kwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura ilieleza wiki iliyopita kuwa bado inasubiri ufafanuzi wa Fifa ndipo itakapomwidhinisha mkali huyo wa kufumania nyavu kuutumikia mkataba wake wa miaka miwili na nusu aliousaini Yanga.

Pengine, lengo la TFF kusimamisha usajili wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba, ni zuri kwa kuwa limelenga kuiepusha Yanga kukumbana na rungu la kuadhibiwa na kukatwa pointi katika mjashindano inayoshiriki kwa kuwa bado kuna kesi Fifa zinazomhusu Okwi.

Aidha, Fifa kupitia kwa msemaji wake, Alois Hug lilikaririwa jana likikiri kupokea barua ya TFF na litatoa ufafanuzi kuhusu masuala yote yanayomhusu Okwi muda wowote baada ya kitendo kinachohusika na usajili kuyapitia.

Okwi, aliyeuzwa na Simba kwa mali kauli ya dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 480) kwa ESS Januari mwaka jana, aliingia mgogoro na wawakilishi hao wa Tunisia katika mashindano ya Kombne la Shirikisho barani Afrika mwaka huu na aliruhusiwa na Fifa kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati mgogoro huo ukishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.

SC Villa imeamua kumuuza kwa Wanajangwani ikidai kuwa ameshamalizana na ESS huku Shirikisho la Soka Uganda (Fufa) lililotoa ITC ya uhamisho wake kwenda Yanga nalo likidai kuwa alikuwa mchezaji huru kabla ya kutua Jangwani