Kocha wa Manchester City Manuel
Pellegrini amesema kuwa timu yake ni bora kushinda bingwa mtetezi wa
ligii ya Uingereza Manchester United.
Raiya huyo ya Chile ameongeza kuwa anaridhia rekodi ya Manchester United ila matokeo ya timu hiyo ya David Moyes yanaonesha kuwa kuwa ni vigumu kuifikia Manchester City kwa vyovyote vile.
Manchester City ni ya tatu kwenye jedwali la msimamo wa ligii kuu ya England, alama tatu nyuma ya viongozi Chelsea, wakati Manchester United ikishikilia nafasi ya saba nyuma ya Liverpoool na Tottenham ambayo iko katika nafasi ya tano ilhali Everton ni ya sita.
Wakati huo huo Manchester United watakuwa uwanjani dhidi ya Olympiakos ya Ugiriki katika ligii ya klabu bingwa barani ulaya.