come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

KIVAZI CHA MAMA BALOTELLI WA TZ CHAZUA UTATA

Baadhi ya wachangiaji katika ukurasa wa facebook wamekasirishwa na mavazi ya mama Balotelli wa Tanzania Beatrice wa Kariakoo wakati akiadhimisha siku ya kuzaliwa ya mwanaye huyo Balotelli wa Tz aliyetimiza miaka miwili.

Katika sherehe hiyo mama Balotelli alionekana akiwa amevaa sketi fupi huku nguo yake ya juu ikiyaacha matiti wazi na kuzua utata.

Mmoja kati ya wachangiaji katika ukurasa wa facebook alisikika aking'aka na kudai kuwa sheria ya Uganda kama ingetumika hapa kwetu basi mama huyo angekutwa na hatia.


Hata hivyo gazeti hili lilipozungumza na mama Balotelli wa Tz ambaye amekuwa akihit kwenye vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii amedai anashangazwa na taarifa hiyo.

Anasema hakuvaa nguo ya kushangaza katika sherehe hiyo isipokuwa sehemu ya matiti iliyoonekana ilitokana na yeye kuinama na ndipo mpiga picha alipopata nafasi ya kumpiga wakati akimlisha keki mwanaye.


'Nilikuwa namlisha keki Balotelli, unajua yule ni mtoto hivyo ni mfupi lazima niiname ili anilishe au nimlishe, kuhusu sketi fupi hilo sikubaliani nalo tena nashangaa, mimi najiheshimu sana siwezi kuvaa vibaya mbele ya jamii' alijitetea.