come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

LUHENDE, BARTHEZ KUSALIA YANGA

Na Regina Mkonde


Yanga iko mbioni kumalizana na nyota wake wawili ambao ilisemekana wako mbioni kuihama timu hiyo kufuatia mikataba yao kumalizika, lakini taarifa za ndani za klabu hiyo zinasema kuwa Alli Mustapha 'Barthez' na David Luhende wanaongozewa mikataba yao hivi karibuni.


Taarifa hiyo ilitolewa na mtu wa karibu wa Yanga inasema kuwa Barthez anahitajika na Yanga kwakuwa bado ni kipa mzuri na uwwake unafanana na ule wa Deogratus Munishi 'Dida' ambaye kwa sasa ndiye Tanzania One.

Pia kiwango cha Luhende kiko juu na ataisaidia Yanga katika mechi zake zijazo za ligi kuu bara na michuano ya kimataifa, taarifa hiyo inasema muda wowote kuanzia sasa nyota hao watasaini tena kuichezea Yanga lakini chanzo chetu kimegundua kuwa kila mmoja atamwaga wino mwaka mmoja.

Kusajiliwa kwa wachezaji hao kumetokana na fununu kuwa watasajiliwa na Simba kwakujwa viwango vimewarirdhisha,hivyo Yanga ikaona ni bora iendelee nao na msimu ujao wataendelea kuvaa jezi za Yanga, kwa sasa nyota hao wanajifua mchangani baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya 2013/14 na Azam fc kutwaa ubingwa