come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

JAJA ASAINI MIAKA MIWILI YANGA, KIIZA AU OKWI KUKATWA

HATIMAYE mshamabuliaji Geilson Santos Santana "Jaja" raia wa Brazil amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016) kuitumikia timu ya Yanga kwa ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.


Katibu mkuu wa Yanga Bw Beno Njovu amesema usajili wa Jaja unakua ni wa pili msimu huu kwa wachezaji wa kimataifa baada ya awali kumsajili kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia ni raia wa Brazil.


"Kazi yetu uongozi ni kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi" alisema Beno.


Jaja ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa Aracaju nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Yanga alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.

Mshambuliaji huyo mwenye mwili uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu katikati ya wiki iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake Leonado Neiva ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha Yanga kwa ajili ya michuano mbalimbali.