MWANA Hip hop chipukizi Dogo Tano ambaye maskani yake mjini Morogoro amefunguka kuwa aliwahi kulizwa katika studio ya Burn Record zilizokuwepo Tabata jijini inayomilikiwa na Sheddy Clever kiasi cha shilingi laki moja za Kitanzania baada ya kuambiwa wimbo wake atafanya na Ney wa Mitego.
Akizungumza kupitia ukurasa wake wa facebook, Dogo Tano amesema Sheddy Clever ambaye ndiye prodyuza aliyegonga wimbo wa Diamond Plutinumz uitwao My Number One na kuweza kushinda katika tuzo mbalimbali nchini na nje ya nchi alihusika moja kwa moja katika utapeli huo.
Anadai alitengeneza wimbo wake huo baada ya kupewa msaada wa kifedha na marafiki zake waishio Morogoro ambapo aliambiwa akatengenezee kwa Sheddy Clever kutokana na ubora wake, Dogo Tanoa anadai alipofika kwa Sheddy alizungushwa karibu miezi kadhaa na alipoingiza voccal alitakiwa kulipa laki moja ili apatikane Ney wa Mitego kwani wimbo huo utanoga zaidi ikiwepo sauti ya Ney.
Hata hivyo Dogo alijikunja na kutoa mkwanja huo na kutakiwa asubirie ngoma yake baada ya Ney kuingiza sauti, hata hivyo alikabidhiwa wimbo huo na kuambiwa sauti ya Ney wa Mitego imeingizwa, lakini alipoisikilizisha kwa jamaa zake na wadau mbalimbali akiwemo mtangazaji mmoja wa redio aliambiwa hakuna sauti ya Ney wa Mitego na kijana umepigwa changa la macho.
Anasema baada ya kupigwa changa la macho aliamua kuonana na prodyuza huyo lakini akawa anazungushwa kilamara anapokwenda na kuambiwa jamaa ametoka, Dogo Tano kwa sasa ameamua kuachana na muziki na kufanya shughuri nyingine lakini amedai hatosahau kamwe jinsi alivyolizwa.
'Sitasahau
nilivyotapeliwa hela zangu ktk studio za burn record zilizokuwa tabata
chini yake sheddy clever. nililipa gharama za kurekodi wimbo mmoja ila
nilitaka niimbe na ney wa mitego. sheddy alinikubalia ila aliniambia
nimpe laki ili ney aingize vocal. nilimpa laki, chakushangaza nikawekewa
sauti feki ya ney. mpaka sasa sina hamu na maprodyuza' alilalamika