Sasa imebainika kuwa baadhi ya wanariadha wa Kenya hawana vifaa vya michezo.
Naibu kiongozi wa ujumbe wa Kenya Tecla Lorupe amesema kuwa wao walifahamishwa siku ya Alhamisi kuwa baada ya wanariadha hawajapokea vifaa na sare zao za michezo.
Lorupe ambaye, ni bingwa wa zamani wa dunia katika mbio za masafa marefu za Marathon, amesema wao wameshangazwa sana na tukio hilo.
Aidha amesema nusura mabondi wa Kenya wakose kushiriki katika mashindano ya mwaka huu, kutokana na ukosefu wa vifaa vyao.
Lorupe amesema walipata bahati wakati, kamishna wa michezo nchini Kenya Gordon Oluoch alipolazimika kutumia fedha fedha zake kununua vifaa hivyo ambavyo vilitumika na mabondia siku ya Ijumaa.
Siku ya Alhamisi, muogeleaji wa Kenya Jason Dunford aliondolewa katika shindano ya mita hamsini butterfly, kutokana na kile alichokitaja kama kutopata vifaa kwa wakati unaofaa.
Mbali na wanariadha kukosa vifaa na mavazi yao, wasimamizi wa michezo mbali mbali nao wanalalamika kuwa hawajapata marupurupu yao.
Hali hii imelleta wasi wasi katika kambi ya kenya huku baadhi ya wanariadha wakiondolewa mapema katika mashindano ya mwaka huu.