come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MAN UNITED WAVUNJA REKODI KUMSAINI DI MARIA

Angel Di Maria 

Manchester United wamekubali kutoka kitita kitakachoweka rekodi ya usajili wa mchezaji kwenye visiwa vya Uingereza kupata huduma zake nyota wa Argentina, Angel Di Maria, kwa dhamani ya pauni milioni 59.7 (dola milioni 98, euro milioni 75).

Di Maria tayari amewasili kwenye makao yao makuu ya Carrington kukamilisha uhamisho wake kutoka miamba wa Uhispania, Real Madrid, kujiunga na mabingwa hao mara 20 wa ligi ya Uingereza.

Vyombo vya habari Uingereze ikiwemo shirika la serikali, BBC, viliripoti kuwa United walikamilisha makubaliano ya kusaini Di Maria baada ya siku kadhaa za mazungumuzo ya hali ya juu na Real.

Inaaminika Di Maria atatia sahihi kandarasi ya miaka mitano itakayo mlipa donge none la pauni 200,000 kila wiki.


Gharama ya Di Maria imevunja rekodi ya awali iliyoshikiliwa na Chelsea ambao walimimina pauni milioni 50 kumsajili straika Fernando Torres kutoka Liverpool mwakani 2011.
Mara ya mwisho wa United kuvunja rekodi ya Uingereza ilikuwa ni 2002 walipolipa Leeds pauni milioni 29.1 kumsajili mlinda ngome Rio Ferdinand ambaye aliondoka Old Trafford kujiunga na QPR mwisho wa musimu uliopita.

Taarifa za kusaini Di Maria kumewapasha moto mashabiki wa United ambao hawajajua linguine isipokuwa majonzi baada ya kushuhudia timu yao ikikosa kutetea taji la Premier na kumaliza wa saba musimu jana.
Nyota huyo wa Argentina aliibuka miongoni mwa wachezaji kumi bora katika Kombe la Dunia kulingana na shirikisho la kandanda duniani, FIFA na alikuwa mchezaji bora wa fainali ya ligi ya mabingwa ya Ulaya baina ya Real na watanashari wao Atletico mwezi Mei.