come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

PHIRI NA SIMBA YAKE WAINGIWA MCHECHETO NA JESHI LA YANGA ZANZIBAR

KOCHA Mkuu wa Simba SC Mzambia Patrick Phiri ameonyesha kutishwa na kikosi kipya cha Yanga kinachonolewa na Mbrazil Marcio Maximo ambao wameweka kambi yao visiwani Zanzibar, Simba na Yanga zimekutana katika mji mmoja wa Unguja, awali Yanga ilikuwa Pemba.

Kocha huyo wa Simba ambaye amerejea tena kuinoa timu hiyo baada ya kumtupia virago aliyekuwa kocha wao Mcroatia Zdravko Logarusic, ametishwa na makali ya wachezaji wa Yanga hasa Andrey Coutinho ambaye alionekana kumfuatilia mara kwa mara.


Yanga ilicheza jioni kabla ya Simba ambayo ilicheza usiku katika uwanja huo huo wa Amaan, katikamecho ya kwanza iliyokutanisha Yanga na Shangani ambayo inashiriki ligi daraja la pili Unguja, Yanga ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa na Coutinho na Telela, katika mchezo huo Phiri alitumia muda wake kuisoma Yanga ambayo ilichezesha vikosi viwili kama kawaida yake.

Yanga ilicheza soka safi la kuvutia uku umahiri wa viungo vwake Haruna Niyonzima, Andrey Coutinho na Hassan Dilunga ulionyesha kumshtua Phiri ambaye muda wote alikuwa ameshika kichwa huku akiuliza ubora wa nyota hao unamtisha, Simba na Yanga zitakutana katika mchezo wa ligi kuu Oktoba 12 mwaka huu.

Usiku Simba ilishuka dimbani kuchezana Kilimani City timu inayoshiriki ligi daraja la pili kanda ya Unguja lakini kiwango cha wachezaji wake kilizidi kumuumiza kichwa Phiri ambapo aliamua kubadili wachezaji wengine lakini hali ilionekana ile ile, Simba ilishinda 2-1 magoli yao yakifungwa na Haruna Chanongo na Shaaban Kisiga kwa njia ya penalti.