|
|
Viongozi Chelsea walufungua mwanya kileleni cha
ligi ya Premier ya Uingereza huku washindani watarajiwa wa taji hilo,
Liverpool, wakianguka nyumbani kwa mshtuko mikononi mwa Aston Villa
katioka mkusanyiko wa matokeo ya Jumamosi.
Mshambuliaji wa Villa, Gabriel Agbonlahor, alifunga goli la pekee ugani Anfield katika dakika ya 9 kutoka hatua chache baada ya mpira wa kichwa wa beki Phillipe Senderos ulipozuiwa na Javier Manquillo na kumwangukia.
Baada ya wachezaji wapya Adam Lallana na Mario Balotelli kukosa shabaha na kutupa nafasi wazi nje, meneja Brendan Rodgers alileta chipukizi matata wa Uingereza, Raheem Sterling kuokoa jahazi bila mafanikio huku nafasi karibu zaidi ya kusawazisha ikiangukia Philippe Coutinho aliyegonga kisingiti cha goli.
Ingawa matokeo hayo yalisababisha mtetemeko, Villa hawajaonja kichapo Anfield tangu 2010 na hawajashindwa tangu mwanzo wa ligi hiyo huku wenyeji wakibaki kulamba maumivu vya kupoteza mechi ya pili muhula huu.
“Wachezaji wangu walipeana kila kitu lakini tulikosa ubora wa kupata goli kwenye thuluthi ya mwisho uwanjani na Aston Villa walidhibiti ngome yao kwa ustadi,” Rodgers alisema baada ya pigo hiyo.
Villa walipanda nafasi ya pili, alama mbili nyuma ya Chelsea ambao waliinuka kutoka kupokea bao la kwanza nyumbani Stamford Bridge kuwakomesha Swansea 4-2 huku straika wao maarufu aliyejiunga nao kabla ya mwanzo wa kampeni hii, Diego Costa, akiendelea kugonga vichwa vya habari kwa kuezeka mabao matatu kimyani.
Wenyeji walianza mechi hiyo kwa fedheha ya nahodha wao John Terry, kujifunga mwenyewe kutoka krosi ya Neil Taylor dakika 11 baada ya boli kuanza lakini Costa alihakikisha wapinzani hao waliingia mapumziko nguvu sawa baada ya kufunga lake la kwanza ilipogonga dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza.
Mshambuliaji huyo sumu alifunga magoli mawili ndani ya dakika 11 za kipindi cha lala salama kupatia vijana wa Jose Mourinho udhibiti, alipotinga kutoka pasi yake Cesc Fabregas kwa la pili na kisha kubadilisha mwelekeo wa kombora lake Ramires lililokuwa linatoka nje wavuni kwa lake la tatu kwenye mechi hii na la saba kwenye msururu wa Premier.
Alipoondoka uwanjani kupumzishwa naye straika wa Ufaransa, Loic Remy, kwa nderemo, Chelsea walipata uongozi wa 4-1 kutoka mshambuliaji wao mpya aliyewachezea kwa mara ya kwanza kabla ya Jonjo Shelvey kuzua hamaki ya muda alipofungia Swansea la pili lakini wenyeji waliweza kukamilisha ushindi.
Kwingineko, Romelu Lukaku na Kevin Mirallas walipatia Everton ushindi wao wa kwanza musimu huu ugenini West Brom katika kivumbi kilichoishia 2-0.
Vijana wapya wa daraja hili Leicester, walisherehekea pia ushindi wao wa kwanza walipolaza wenyeji Stoke 1-0 kupitia shujaa wao Leonardo Ulloa.
Tottenham Hotspur walilazimishwa sare ya 2-2 ugenini Sunderland wakati Harry Kane alijifunga dakika nane kabla ya mechi kukatika.
Mshambuliaji wa Italia, Graziano Pelle, alifunga magoli mawili na kusaidia Southampton kuwaadhibu Newcastle 4-0 na kuongezea mwalimu wao, Alan Pardew, anayetishiwa na kufutwa kazi kufuatia matokeo duni.
Burnley waliopanda daraja musimu huu walikosa penalti kwenye sare nuge ugenini Crystal Palace.