Manchester United wamekubali kusaini mshambuliaji hatari wa Colombia, Radamel Falcao kwa mkopo wa musimu mmoja kutoka Monaco katika tukio ambalo limetetemesha ulimwengu wa soka Jumatatu.
United walifanikiwa kushawishi Falcao, 28, kutupia Ream Madrid, Manchester City na Arsenal kisogo kujiunga nao kwenye mkataba utakao wagharimu pauni milioni 6 wenye chaguo la kukamilisha usajili wa kudumu mwisho wa musimu.
Falcao aliyekosa Kombe la Dunia alipoumia goti atakamilisha uhamisho huo baada ya vipimo vya kimatibabu na kukubaliana ajira na United.
Amefunga magoli mawili katika mechi tatu baada ya kuuguza jeraha lake kuendeleza sifa zake kama mojawepo wa mshambuliaji hatari zaidi mbele ya lango ulimwenguni.
Falcao, ambaye amefungia Colombia magoli 20 katika mechi 50 ametinga mabao 200 akichezea Atltico Madrid na Monaco na aliwachwa nje kutoka kikosi cha timu yake wikendi iliyopita ambapo walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Lille.
Kumsajili kwake ni ishara kuwa Uinted, ambao walidorora musimu jana na kumaliza wa saba katika utetezi wa taji la ligi ya Premier ya Uingereza, wananuia kurejea kileleni kwa kishindo muhula huu chini ya utawala mpya wa meneja Louis Van Gaal.
Tayari mwalimu huyo amemimina pauni 130 milioni, historia ya klabu hicho, kuwasajili viungo maahiri watakao fanikisha azima yake kurejesha United mahala pao kama magwiji wa Uingereza na Ulaya.
Walivunja rekodi ya usajili ya Uingereza majuzi kwa kumsaini Angel Di Maria kutoka Real Madrid kwa ada ya pauni milioni 59.7.