|
|
Nyota wa Brazil, Neymar, alitoka benchi na
kufunga magoli yote mawili yaliowezesha majitu wa Uhispania, Barcelona,
kuandikisha ushindi wa tatu mtawalia kwa kunyuka Athletic Bilbao 2-0
kwenye ligi kuu ya Uhispania, La Liga, Jumamosi.
Ushindi huo uliendeleza mwanzo mwema kwa mwalimu wao mpya na nahodha wao wa zamani, Luis Enrique, ambaye bado kuonja kichapo au sare katika mechi zake tatu za kwanza kwenye shindano hilo.
Neymar alipumzishwa baada ya kurejea kutoka safari ndefu Marekani kuchezea taifa lake ambalo lililaza Colombia na Equador ndani ya juma lililopita lakini aliibuka shujaa na kuleta tofauti baina ya timu hizi zilizochuana uso kwa uso.
Ikisalia dakika 11 muda wa kawaida kutimia, Neymar alipokea pasi kutoka nyota mwezake wa Argentina, Lionel Messi, na kufunika boli wavuni bila kusita.
Dakika tano baadaye, wawili hawa walizua taharuki ngomeni ya Bilbao na kufanikiwa kupatia Barcelona la pili baada ya Messi kuwachenga mabeki watatu na kukata mpira nyuma kisandukuni kumuunganishia Neymar fursa ya kutia kizimbani ambayo hakutupa.
Barca wanasalia kileleni cha La Liga, alama tano mbele ya mabingwa Atletico Madrid na sita mbele ya watanashari wa mikaka, Real Madrid, kabla ya mechi kali baina ya majirani hao baadaye Jumamosi.
“Messi ndiye bora zaidi duniani. Yeye ni nyota na ninaendelea kuimarika kwa kucheza pamoja naye,” Neymar alisifu kigogo mwenzake baada ya mechi.