come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

RODGERS AFURAHIA MATOKEO YA JANA

Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, ametiwa moyo na ukakamavu wa timu yake baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa 2-1 dhidi ya klabu cha Bulgaria, Ludogorets Razgrad, waliporejea ligi ya mabingwa baada ya miaka tano Jumanne.

Mabingwa hao mara tano wa taji hilo walihitaji penalti sekunde za mwisho za muda wa ziada kukomesha hima ya wageni wao baada ya Dani Alabo kukomboa bao lake nyota Mario Balotelli aliyefungia Liverpool la kwanza tangu kujiunga nao mwezi jana kutoka AC Milan dakika ya 82.


“Hili ni shindano la ushindi na kushinda mechi. Wakati mwingine, unacheza vyema bila kupata matokeo na ni muhimu kwetu kurejea katika shindano hili na ushindi,” Rodgers alizungumza baada ya mechi hiyo.

“Tulionesha utulivu na ukakamavu ulio kwenye kundi hili huku mashabiki wetu wakishangilia kwa shime. Hatuko kwenye kiwango cha musimu jana kwani wachezaji wengi hapa ni wapya na wanaendelea kupata uzoefu wa mbinu zetu,” mwalimu huyo aliongeza.